Monday 9 September 2013

MTANDAO WA WIZI WA FEDHA HALMASHAURI

  IMEGUNDULIKA kuwapo na mtandao hatari nchini unaohusisha Hazina na Halmashauri mbalimbali kuchota mamilioni ya fedha huku wakiziandikia kutumika katika miradi ya maendeleo. Mtandao huo ambao umeelezwa kuwahusu viongozi ngazi ya juu wa Hazina na Halmashauri umekuwa ukiongeza fedha za ziada kati ya Sh. Milioni 500 hadi 600 kwenye fedha halali za miradi ya maendeleo zilizoidhinishwa kisheria na Bunge. Tayari mtandao huo umedaiwa kufanikiwa kuidhinisha mamilioni ya fedha katika Halmashauri tatu ambazo ni Mbarali, Korogwe Mjini na Mvomero. Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Rajab Mohamed Mbarouk alipokuwa akifanya majumuisho ya vikao vya kamati yake. Mbarouk alisema kumeibika mtandao hatari wa kujichotea fedha za Serikali kwa kusingizia zinakwenda Halmashauri lakini zinapofikishwa huko zinawarudia wenyewe. “Hii nchi sio masikini na hakuna sababu ya kusikia eti miradi imekwama kwa sababu ya fedha kukosa, katika vikao vyetu tumebaini kwamba Hazina na Halmashauri nchini zinashirikiana kula fedha za Serikali. “Mfano halisi ni huu Halmshauri ya Mbarali katika mahesabu yamahitaji yao yote walitakiwa kupewa Sh. milioni 70 lakini Hazina walipeleka Sh. milioni 700. “Fedha hizo zinapofikishwa kule zinaidhinishwa kupokelewa Sh. milioni 70 zilizokuwa zikihitajika zile zilioongezwa zinazrudi mikononi mwa mtandao huo ambao ni katika Hazina na Halmashauri. “Halmashauri ya Mbarali imekuwa imekuwa ikipata hati chafu mpaka leo ninavyoongea hapa katika kuboroga kwenye mahesabu yao ya fedha wanazopokea na jinsi wanavyozitumia. “Kama unataka kuona mtandao huo umeota mizizi mikubwa, tumebaini utakaswaji wa fedha umefanyika Halmashauri ya Korogwe Mjini Sh.milioni 500 huku mahitaji yao yakiwa chini ya Sh. milioni 100. “Hivyo hivyo utakaswaji huo umefanyika Halmshauri ya Mvomero kwa kupelekea Sh. milioni 500 ambapo mahitaji yao hayakuwa yanafikia kiasi hicho, kama wana kamati tumechukizwa na utoroshwaji wa fedha hizo na tutalifikisha bungeni kwa hatua zaidi. “Cha ajabu unakuta viongozi wanaohusika katika Halmashauri hizo wanapofanya utakaswaji huo wanawahi kuhama, mfano halisi ni aliyekuwa Mhasibu wa Halmshauri ya Mvomero,Nassoro Mkwanda ambaye hivi sasa yupo Halmshauri ya Kiteto kwa cheo hicho hicho,”alisema. Mbarouk alisema kama mtandao huo hautadhibitiwa haraka taifa litaendelea kufilisika na maendeleo ndani ya jamii yakikwama ambapo athari yake ni uchumi kushikiliwa na wachache huku kundi kubwa ni masikini. Mkurugenzi Kiteto amwaga machozi Awali ya yote, Kamati ya LAAC ilikutana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kupitia mahesabu yao ambapo ilikubaini ubadhirifu mkubwa wa fedha kitendo kilimfanya Mkurugenzi halmashauri hiyo, Jane Mutagurwa kulia ndani ya kikao. Kugundulika kwa ubadhiri katika Halmshauri hiyo kulimfanya Mwenyekiti wa LAAC, Mbarouk kuagiza polisi kufika hapo ili kuwaweka chini ya ulinzi baada ya kikao kumalizika. Kamati ilibaini Halmashauri ya Kiteto imepoteza Sh. milioni 500 ambazo ambazo ni mapato ya kodi za mazao kutoka kwa vyama vya ushirika. Ilibainika fedha hizo zilichukuliwa na wakala wa ukusanyaji wa ushuru huo kwa idhini ya Halmashauri hilo kwa mkataba wao lakini wakotomea bila kuzikabidhi. Katika mahojiano kati ya wabunge wa kamati ya LAAC na viongozi wa Halmashauri hiyo ilibainika kuwa kuna magari mawili ya Serikali yenye usajili wa STK hayajulikani yalipo na anayeyamiliki licha ya kuonekana kwenye vitabu vyao ni mali zao. Pia ilibainika kuwa Sh. milioni 179 zimeanzwa kulipwa kwa watumishi wanaoidai Halmashauri hiyo lakini hawajulikani kwa majina wala idara zao. Vile vile imegundulika kwamba Halmashauri hiyo imekutumia Sh.milioni 34 zilizotokana na mauzo ya mahindi ya msaada wa njaa iliyoikumba Wilaya ya Kiteto na hazijawahi kurudishwa Ofisi ya Waziri Mkuu. Ubadhirifu mwingine uliopatikana katika Halmashauri hiyo ni ujenzi wa jiko la kisasa lililogharimu Sh. milioni 25 lakini limeshindwa kutumika na badala wameligeuza kuwa nyumba ya mwalimu huku taarifa zao zikieleza vitu vyote vimekwekwa kumbe ni uongo. Hata hivyo ilibainika mamilioni ya fedha yanayotengwa na Serikali kwemnda miradi mbalimbali ya maendeleo vijijini na mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana hayawafikii ipasavyo. Ilibainika miradi mingi ya ujenzi wa shule za msingi na Sekondari ikiwani ya Kiperesi ikishindwa kukamilika huku fedha zilizotengwa zikiwa zimetolewa kitendo ambacho kiliwafanywa wajumbe wa LAAC kupendekeza kuvunjwa kwa Halmshauri hiyo. Wakati Mkurugenzi, Mutagurwa alipotakiwa kutoa majibu ubadhiri huo alipatwa na wasiwasi na kigugumizi kueleza wazi na kuanza kulia. Viongozi wengine waliokuwa wamsaidia kujibu hoja ni Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo,Rabson Magesa, Mwenyekiti wa Halshauri ya Wilaya ya Kiteto, Mainge Lemalali na viongozi wengine ambao ilionekana kumsukimia mkurugenzi wao. Kutokana na kutokuwapo na majibu sahihi, Mbarouk alimua kuwatoa nje viongozi wengine ispokuwa Mkurugenzi ili kuhoji peke yake ambapo ilibainika kwamba viongozi waliomzunguka wanamhujumu huku jamii ya wamasai wakimdharau ni jinsia yake ya kike. Mbarouk aliamua kusiktisha mpango wa kumweka chini ya ulinzi wa polisi baada ya kuelezwa hivyo na kuamua kuunda kamati ndogo ya kuchunguza ubadhirifu na hali halisi ilivyo Kiteto. Pia alipewa muda wa kuhajikisha fedha pamoja na gari mbili zinapatikana kabla ya Disemba 31, mwaka huu ingawa aliomba kuongezewa muda hadi Juni 2014 kitendo kilichopingwa vikali. MWISHO.

WALEMAVU WANAVYOTESEKA DAR ES SALAAM

Siri nzito ya walemavu wanavyoteseka Dar.

 INASIKITISHA na kuleta huzuni ndani ya moyo wako pale unapojikuta unawapoteza wazazi wako wote huku ukikosa msaada kutoka kwa ndugu wa karibu na kuamua kujiunga na kundi la ombaomba barabarani. Baadhi ya watu wanao kuwa wakiomba msaada hasa wale walemavu wa viungo mbalimbali wa mwili wamekuwa wakileta huzuni kwa wapiti njia kutokana na ulemamavu wao ambao ni mipango ya Mungu. Sote ni mashahidi kuwa baadhi ya walemavu wa mikono, miguu, vipofu na viungo vingine wakiomba msaada kwa madereva, watembea kwa miguu na kwenye ofisi za Serikali na binafsi na maeneno mengine. Lakini wapo wengine ambao hawana tatizo lolote lakini wameamua kuingia katika kundi hilo jambo ambalo limekuwa likizua maswali ya kwamba kwanini wasijishughulishe na biashara ndogondogo. MTANZANIA Jumatatu ilifanya mahojiano na mlemavu mmoja wa miguu yote ambaye amekuwa akitembea mithili ya mnyama mwenye miguu minne wakati akiomba msaada katika kituo cha daladala Ubungo. Mlemavu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Yusuph Said (24) mzaliwa wa Kijiji cha Mikese mkoani Morogoro anaeleza maisha anayoishi eneo la Manzese Darajani jijini Dar es Salaam ambayo ni hatari kwa usalama wa uhai wake. Said ambaye alisoma Shule ya Msingi Kitega na baadaye kujiunga na Sekondari ya Mikese zote za mkoani Morogoro anaeleza kwamba alikimbiwa na ndugu zake baada ya wazazi wake wote kufariki 2000 kutokana na maradhi mbalimbali. Akizungumza kwa huzuni ya kuwapoteza wazazi wake ambao walikuwa wanamlea kulingana na hali yake ya ulemavu alijikuta akikosa mtu wa kukaa naye kitendo kilichomfanya kukimbilia kwa shangazi yake Muhombola Salum. Said anasema alikimbilia kwa shangazi yake baada ya ndugu zake wa kuzaliwa tumbo moja kumkimbia na kuanzisha maisha yao maeneo mengina huku shughuli zao kubwa ni kuchoma mkaa porini. Anasema maisha kwa shangazi yake yalizidi kuwa magumu kutokana na kutokuwa na uwezo kwani uhakika wa kula kila siku haukuwapo ambapo alishindwa kuvumilia njaa na kukimbilia Dar es Salaam baada ya kupata taarifa kuwa walemavu wanapata msaada barabarani kwa kuombaomba. Hakika, ukimtazama Said hali yake ni vigumu kuvumilia kumsikiliza au kumwangalia kwani mwili wake unaonekana kutooga siku nyingi, nguo chafu, shuka analojifunika chafu ana anatembea nalo muda wote kwa kuhofia kumwibia. Pia inadhihirisha kabisa ameanza kuathirika kisaikolojia kutokana na mazingira anayoishi na inathihirisha wazi ameanza kutumia dawa za kulevya. Said ambaye alikataa kuweka wazi vitendo wanavyofanyiwa walemavu wanaoishi eneo la Manzese Dar es Salaam nyakati za usiku kwa kuhofia maisha yakwe, anasema anatamani kurudi nyumbani lakini anashindwa wapi atafikia. “Pale Manzese kuna masela wengi sana, wanatufanyia mambo mengi lakini siwezi kuyataja hapa naogopa na ndio maana sisi walemavu tumejitenga na banda letu. “Hii ni shuka ninayojifunika natembea nayo muda wote kwa ukiachaa unaibiwa, kuoga kwangu au kufua nguo hizi mara nyingi ninasubiri mvua inaponyesha. “Mimi nilikuwa nalelewa na wazazi wangu bila kutekeseka na walikuwa wameninunulia baiskeli lakini walipofariki iliharibika na hakuna aliyenitengenezea lakini nashukuru hadi leo naishi kwa msaada wa watu. “Ukiamua kuwahoji wapiga watu tunaolala nje watakueleza mambo mengi sana, kuna vituko tunafanyiwa sio kwmaba tunapenda ni kwa sababu huna jinsi,”anasema kwa masikitiko. Said anasema kwamba kutokana na kukaa kituoni tena juani kwa kuomba pesa abiria, madereva na makondakta amekuwa akiugua kila siku lakini baada ya kupata kiasi hutenga kwa kula chakula na kununua dawa la kutuliza maumivu. Anasema kwamba anahofia kwenda hospitali kutibiwa kwa kile alichodai hatapewa fursa ya kupata matibabu kwa sababu ya pesa na hali yake ilivyo. Anasema kwa siku inaweza kupata Sh 5,000 lakini kutokana na mazingira anayoishi hazitoshi na kuongeza kwmaba pengine hunyang’anywa na masela nyakati za usiku. Anaeleza kwamba mbali ya kunyang’anywa fedha pia kupokonywa simu jambo ambalo linamfanya kutonunua simu, nguo au kutunza fedha za ziada. Anasema kutokana na hali hiyo hulazimika kuchimba shimo na kufukia baadhi ya fedha zake anazopata kutoka kwa watu wanaoguswa na hali yake. Said aliwataja baadhi ya ndugu wa kuzaliwa ni pamoja na Oluka, Salum, Hiari, Shukuru na Hamis ambao wapo porini wakiendesha shughuli zao za kukata miti na kuchoma mkaa mkoani Morogoro. Pamoja na mambo ya Said lakini ombi lake kubw ani kuiomba Serikali kumsaidia baiskeli ya kutembelea au kumpeleka katika kituo chochote za kulelea watu wasio na uwezo. Said anasema mbali ya kumpeleka kituoni, anaomba msaada wa fedha ili kuanzisha biashara ndogo ambazo anaweza kusifanya kwa kutumia mikono ambayo haina ulemavu wowote. Ni dhahiri kwamba Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inapaswa kutambua matatizo yanayowapata watu wanaojihusisha na ombaomba barabarani. Inagawa ni vigumu Serikali kuwachukua watu wote walio mitaani na kuwatunza lakini kuja haja ya kuchukulia uzito kwa watu wenye ulemavu hata kwa kuwapeleka katika vituo vya kulelea watu wasio na uwezo. Si kwamba walemavu wote wanapenda kukaa kwenye vituo hivyo la hasha, bali wengine wanataka kupata msaada wa fedha ili kuanzisha biashara ambayo wanaweza kuifanya kulingana na mazingira yao. Pia Serikali inapaswa kuweka wazi juu ya huduma kwa walemavu katika hospitali za umma ili waweze kupata huduma bure kwa sababu ya hali zao ambazo haziwawezeshi kupata kipato cha kujikimu, hii itasaidia pale wanapougua walemavu waweze kupata matibabu kwa sababu wana haki sawa. Walemavu wanapoachwa bila kupewa huduma ni moja ya sehemu ya kuwafanyia ukatili. Sote tunafahamu ukatili ni vitendo vya makusudi vinavyofanywa na mtu au kikundi dhidi ya mtu, watu wengine ambavyo huwa na madhara ya kimwili, kiakili na jisaikolojia. Dhana hii haimanishi kuuawa kwa binadamu pekee bali ukatili unaweza kujitokeza katika sura tofauti na maneno mbalimbali kama ukatili wa nyumbani, kiuchumi, kimila na desturi katika makabila, mahusiano ya kimapenzi, usafirishaji haramu wa binadamu, vitisho na matumizi ya kutumia nguvu. Hivyo watu walio barabarani wakiomba msaada wa kusaidia wapo katika kundi la ukatili wa kiuchumi ndio uliowafanya kuingia barabarani kujipatia riziki zao. Kwa mujibu wa Said amesema kwamba nyakati za usiku hufanyiwa vitendo vya ajabu ambavyo hakuta kuvieleza wazi, lakini kwa akili ya kawaida inadhihirisha kundi hilo linateseka sana . Ukatili unaweza kutoka katika kundi lolote ndani ya juamii ikiwa ni kwa mwanamke, mwanaume, mvulana, msichana au mototo. Ili kutambua madhara ya ukatili wa kijinsia kwa walengwa hao ni muhimu kufanya linalowezekana kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kuona kila binadamu ana haki katika hali yoyote ile. Ingawa mateso wanayopata walemavu barabarani jamii imekuwa ikiyachukulia pengine ni uamuzi wa mtu kupenda kuingia katika kundi hilo lakini sivyo ilivyo bali inalazimu kutokana na hali halisi ya maisha. Umefika wakati sasa wizara, idara, taassi na kampuni binafsi kuona kundi la walemavu ni moja ya watu wanaopaswa kusaidiwa katika kila hali kwa sababu hayo ni mapenzi ya Mungu. Pia vitendo vya baadhi ya familia kuwatelekeza watoto wanaozaliwa kwa ulemavu au kupata ulemavu wakiwa watu wakubwa ni jambo la kikatili , ni vema mlemavu akadhaminiwa kama ilivyo kwa wengine. Maoni 0769 688 300

UWEZO WA NAIBU SPIKA BUNGENI

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema uwezo wa Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai katika kuongoza Bunge unahatarisha amani, kuvunjika mshikamano na umoja wa kitaifa uliopo sasa kutokana na kutokuwa na mtazamo mpana wa kufikiri. Pia kimesema kuna ajenda ya chini chini inayoendelezwa na baadhi ya mawaziri, wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kiti cha Spika katika kuhujumu malengo na nia ya Rais Kikwete kuwa na katiba mpya ifikapo 2015. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alisema kitendo cha Ndugai kuamuru polisi kumtoa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe ni cha aibu na kidikteta. Profesa Lipumba alisema kuna baadhi ya viongozi Serikali (hawakuwataja) wanaojionesha wanamsaidia Rais Kikwete lakini ndani ya moyo wao wana ajenda za siri za kumhujumu. Alisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakitumia udhaifu wa Ndugai kwa kumshawishi kufanya kile wanachoona kinafaa kwa lengo la kukandamiza upinzania na kuhmhujumu Rais bila yeye kujua. Alisema kuwa hivi Sasa Tanzania inakabiliwa na changamoto za matamshi hasi yanayotolewa na viongozi na asasi za Rwanda baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ushauri wenye mantiki kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kukutana na waasi wa kikundi FDRL kitendo ambacho kimeleta hali ya sintofahamu. Pia alisema kuwa kitendo cha baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kufanya vikao vyao na kuitenga Tanzania huku wakizungumzia namna ya kuinua uchumi wao, kitendo ambacho kinamweka Rais Kikwete katika changamoto kubwa. Alisema kuwa kitendo cha kiti cha Spika hasa kinapokaliwa na Ndugai kimekuwa kikiendesha Bunge kwa kupendelea Serikali kwa kadri kinavyoweza huku kikizima hoja za upinzani kwa makusudi. “Kuna njama za wazi zinafanywa na kiti cha Spika kwa kutelekeza maoni ya wananchi na kupendelea ya Chama Cha Mapiunduzi (CCM), kwa upande wa Zanzibar hawakushirikishwa vizuri na hata wabunge wa CUF wanasema hawakushirikishwa. “Moja ya njama za wazi ni ile ya wabunge 166 wa bunge la katiba wanaoipaswa kupendekezwa na taasisi mbalimbali na kuteuliwa na Rais, sisi CUF kinasikitishwa na mchakato unavyoendeshwa na jinsi uteuzi unavyopendekezwa. “Hii katiba mpya itakuwa ni ya CCM sio ya Watanzania, na ombi la wabunge wa CUF ni kutaka muswada urudishwe kwa wananchi na kamati ijadili upya. “ CUF inaendelea na juhudi za kuwasiliana na viongozi wa vyama vingine ili kuweka mkakati wa pamoja na kukabiliana na hujuma dhidi ya mchakato wa kupata katiba mpya na kuimarisha umoja wa kitaifa,”alisema. Profesa Lipumba alisema kuwa kitendo cha Ndugai kumnyima nafasi Mbowe kinadhihirisha ni mpango mkakati wa kuminya hoja za upinzani na kutumia nguvu kumtoa nje ya Bunge hakikubaliki na amevunja sheria. Profesa Ibrahimu alihoji kwamba angesimama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, je asingepewa nafasi ya kusikilizwa na kuongeza kwamba baadhi ya Wabunge wa CUF akiwamo Mozza Abeid walivuliwa hijabu zao kitendo ambacho ni udhalilishaji.