Ukatili huu utaisha lini Kanda ya Ziwa?
*Mtoto avunjwa mguu kisa anakojoa
ovyo
Na Benjamin
Masese, Mwanza
ILE kauli ya
kwamba ‘Uchungu wa mwana aujuaye mzazi’ inakosa uhalisia wake kutokana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kutokea
maeneo mbalimbali ya nchi.
Sote
tunafahamu watoto ambao ni tegemeo la
taifa la kesho wamekuwa wakikumbana na vitendo vya kinyama vinavyofanywa
na wazazi wao au walezi ambapo hivi sasa wanaonekana kuwa waathirika wakubwa wa kuwatelekeza.
Moja ya
tukio la kusikitisha ambalo liliwaliza
akina mama na watu wengine
walioshuhudia unyama wa mama
Enjoy turukale kumpiga mtoto wake wa kuzaa Teddy Turukale (2) kwa
kutumia vitu vya ncha kali hadi kumvunja mguu.
Kisa na
mkasa cha mama huyo kufanya unyama huo ni tabia ya mtoto huyo kukojoa na kunya
mara kwa mara kitendo kilichomkera na
kuamua kumpa kipigo cha mbwa mwitu bila kujali ni mtoto ambaye ni malaika anayetenda
jambo asilojua.
Mtoto
Teddy alifanyiwa ukatili na mama
yake mwanzoni mwa Januari mwaka huu
akiwa nyumbani kwake Kisesa jijini
Mwanza kwa kupiga na kitu cha ncha kali eneo la paja.
Hata hivyo
baada ya tukio hilo mama huyo aliamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa Bugando
na kuombwa PF3 na madaktari ili aweze kutibiwa kitendo
kilimchomfana mama huyo amtoroshe
hospitalini hapo na kumtekeleza kwa bibi yake Tereza Turikali eneo la Pasiasi.
Hata hivyo
kutokana na mguu wa mtoto huo kuoza na kutoa harufu kali kutokana na kutibiwa na mganga wa kienyeji
akimuosha kwa dawa ya maji aina ya JIK, mguu uliendelea kuoza.
Kutokana na
harufu kuenea mtaa mzima, majirani walianza kujiuliza maswali na hatimaye
kubaini kuna mtoto amefichwa ndani kwa
bibi Tereza ambaye ni jirani yao na kutoa taarifa kwa uongozi wa Serikali za
Mtaa wa Pasiasi Juu, polisi na kituo cha kuokoa maisha ya watoto waliofanyiwa
ukatili.
Kutokana na
hali hiyo MTANZANIA iliamua kuafutailia
tukio hilo katika ngazi zote ili kujua hatma ya mtoto huyo baada ya kugundulika
akiwa amefichwa ndani ya nyumba ya bibi
Tereza.
Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa
wa Pasiasi Juu, Merry Joseph anasema baada ya kupata taarifa kutoka kwa
wananchi wake aliwaita polisi na watumishi wa Kituo cha uokoaji watoto cha
Foundation Karibu Tanzania (FKT) pamoja a polisi jamii na kuvamia nyumba hiyo.
Anasema kama
mzazi alishindwa kuvumilia na kuanza kulia kutokana na jinsi mtoto alivyokuwa
ameoza mguu huku ukiwa mweusi mithili ya mkaa (kama picha inavyoonekana).
Joseph
anasema baada ya kumuokoa mtoto huyo walimkabidhi kwenye kituo cha FKT, polisi kwa hatua zaidi ya matibabu na sheria.
Pamoja na
mambo mengi lakini anasema kwamba ukatili dhidi ya watoto unaendelea kufanyika
kutokana ugumu wa maisha na baadhi ya wazazi kutokuwa na elimu nzuri juu ya
malezi na makuzi ndani ya familia zao.
Pia anasema
asilimia kuwa ya wazazi wamekuwa wakiwafanyia ukatili watoto wao lakini
hukimbilia kwa waganga wa kienyeji kuwatibu badala ya hospitali kw akuhofia
kukamatwa.
MTANZANIA
ilifanikiwa kufanya mahojiano na Mjumbe wa Mtaa huo, Juma Fadhili, balozi wa shina 75 wa CCM, Mariam
Twaha na polisi jamii wa mtaa huo, Joseph Sigareti ambao walifanikisha kufichukuliwa
kwa mtoto huo ambapo walisema wamesikitishwa na unyama huo.
Kwa upande
wa Mwezeshaji wa kituo cha FKT, Abimerick Richard anasema baada ya uvamizi
ndani ya nyumba ya bibi January 17 mwaka huu, siku ya pili yake walikabidhiwa
mtoto huyo na kumpaleka Hospitali ya
Sekou Toure huku mguu ukiwa umeonza.
Anasema hata
hivyo walishindwa kumtibu ndipo walipopelekwa Hospitali ya Sengerema DDH ambayo
ina wataalamu na kukatwa mguu Januari
19, 2014 na kukatwa mguu kama inavyoonekana kwenye picha.
Anasema
kwamba hadi sasa mtoto huyo bado anaendelea na matibabu na gharama zote wanatoa wao.
Katika suala
la ukatili, anasema kwamba jamii
inachangia vitendo vya kinyama kuendelea kutokea kutokana na kuficha
taarifa na kuona jukumu hilo ni la
Serikali pekee
Pia
anaongeza kuwa vyombo vya dola vinachangia kwa kupindisha sheria hasa pale
inapogundulika mwenye fedha au kigogo amefanya ukatili dhidi ya mtoto wake.
Kwa upande
wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nyamagana hadi sasa linaendelea kuwasaka wazazi wa
mtoto Teddy kwa kuwa hawajulikani walipo na bibi aliyekutwa na mtoto huyo
anaendelea kuhojiwa.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, Jalia Mtani anasema tafsiri ya ulinzi ni kulinda kitu au kiumbe ili kisidhurike kwa
namna yoyote ile.
Anasema kwa
upande wa mtoto anapaswa kulindwa ili asiweze kunyanyaswa, kufanyiwa ukatili wa
aina yoyote ile huku akitoa mifano kwamba sheria ya mtoto ya 2009 inakataza
mtoto kutokwenda baa, kuagizwa sigara, kunywa pombe na ikibainika mzazi
amekwenda naye katika mazingira hayo anatozwa faini ya Sh milioni moja hadi
nne.
Mtani
anasema kitendo cha watoto kuwapo mitaani ni sehemu ya ukatili unaosababishwa
na wazazi kutokana na kutoelewaza au nyumba kukosa amani.
Anasema
chanzo cha ukatili ndani ya familia ni usongo wa mawazo moyoni, hasiara,
umasikini ambao unasababisha baadhi ya wazazi kutelekeza watoto na kuongeza
kuwa familia isiyo na upendo lazima vitendo hivyo vitatokea.
Anasema
Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuacha vitendo hivyo na kufuata
sheria zinavyoelekeza, hata hivyo aliongeza kuwa sheria zipo za kuadhibu mtoto
kama amekosea.
Naye Padri
wa Kanisa Katoliki la Nyarubere Jimbo la Geita Wilaya ya Nyanghwale, Thomas
Kabika Mbilingi anasema vitendo vya ukatili ni unyama, mmomonyoko wa maadili,
uvunjifu wa amri za Mungu, jamii, Serikali na jumuiya.
Padri Mbilingi
anasema ukatili ni ukosefu wa upendo wa mtu kwa mtu, mtu kwa Mungu (Mathayo
7:12) inasema unayotaka kutendewa wewe watendee wenzako, (Yohana 1:34) inasema amri mpya nawapeni ni
agizo na fundisho la Yesu kwa ufuasi wake.
Anasema
sababu za kutokea ukatili kwa watoto ni jamii au mtu binafsi asiye na upendo,
maadili, utu lazima atatenda ukatili.Anaongeza kuwa Serikali, jamii kutokazia
amri na sheria kwa wananchi juu ya
uhalifu na kusababisha ukatili kuongezeka.
Padri
Mbilingi anasema ubinafsi unaonekana kutawala zaidi kuliko ujamaa ambao unaleta
ukatili, pia anabainisha kwmaba watu wanaonekana kuacha dini ya mafundisho ya
Yesu Kristo wa agano jipya na badale yake wanafuata agano la kale.
Anafafanua
kwamba mafundisho ya agano la kale linaekeleza kuwa jina kwa jino yaani
ukitendewa na mtu vibaya lipiza lakini agano jipya linafundisha kufuata
maandiko ya Yesu ambaye anasema adui wako mpende.
Padri
Mbilingi anasema ili kuzuia ukatili dhidi ya watoto lazima mafundisho na
msisitizo ukaziwe popote kanisani, msikitini, mihadhara na kuongeza wahalifu
wachukuliwe hatua.
Hata hivyo
mwanasheria wa Kujitegemea , Abimerick Richard anasema sheria zilizopo hazitoi
adhabu kali kwa wanaofanya ukatili wa watoto na kuitaka Serikali kuboresha
sheria zake kwa kuongeza adhabu kali.
Kutokana na
matukio ya ukatili ni muhimu Serikali
kuunganisha nguvu pamoja na taasisi zinazopinga vitendo hivyo zikiwamo Mtandao
wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN).
Mtandao wa Tecden ni umoja wa watu na asasi ambao kwa pamoja wana nia ya kuunganisha sauti zao ili kuleta hamasa na mchango katika sera na programu zinazohusu malezi, makuzi na maendeleo ya watoto wadogo kwa kubadilishana habari, uzoefu na ufahamu katika malezi, makuzi na maendeleo ya watoto wadogo.
Kwa kuwa dira ya mtandao huo ni kuwa na ukakika wa taifa ambalo watoto wote tangu kutungwa mimba hadi miaka minane wanatunzwa na kulelewa vizuri kwa kupata haki za haki zao za msingi za kuishi na kukua vema .
Ni wakati muafaka sasa Serikali kuunganisha dhamira yake na kuunga mkono taasisi za namna hiyo katika kufanikisha ukatili nchini unakwisha.
Ikiwa Serikali itaungana pamoja na FKT, Tecden na nyingine za namna hiyo, hakika watafanikisha kujenga mazingira bora ya kujengeana uwezo ili kuwezesha sera na programu za maendeleo katika ngazi zote ili kuleta msukumo wa kuboresha huduma za maendeleo kwa watoto wadogo.
Mtandao wa Tecden ni umoja wa watu na asasi ambao kwa pamoja wana nia ya kuunganisha sauti zao ili kuleta hamasa na mchango katika sera na programu zinazohusu malezi, makuzi na maendeleo ya watoto wadogo kwa kubadilishana habari, uzoefu na ufahamu katika malezi, makuzi na maendeleo ya watoto wadogo.
Kwa kuwa dira ya mtandao huo ni kuwa na ukakika wa taifa ambalo watoto wote tangu kutungwa mimba hadi miaka minane wanatunzwa na kulelewa vizuri kwa kupata haki za haki zao za msingi za kuishi na kukua vema .
Ni wakati muafaka sasa Serikali kuunganisha dhamira yake na kuunga mkono taasisi za namna hiyo katika kufanikisha ukatili nchini unakwisha.
Ikiwa Serikali itaungana pamoja na FKT, Tecden na nyingine za namna hiyo, hakika watafanikisha kujenga mazingira bora ya kujengeana uwezo ili kuwezesha sera na programu za maendeleo katika ngazi zote ili kuleta msukumo wa kuboresha huduma za maendeleo kwa watoto wadogo.
0683 608 958
MWISHO.