Wednesday, 19 February 2014

VIONGOZI WA SERIKALI WANAPODIRIKI KUFANYA UBAGUZI OFISINI



Itikadi, ubaguzi wa RC Ndikilo Mwanza unahitaji dawa haraka
*Makada wa Chadema waanza kusakwa Serikalini
Na Benjamin Masese, Mwanza
WAKATI tunafikiria uhasama unaoendelea kati ya wafugaji na wakulima nchini kufikia hatua ya kuuana kama wanyama ,inaonekana wazi kuna baadhi ya viongozi wa Serikali wanafanya kazi kwa ubaguzi na itikadi za kisiasa.
Ni jambo la hatari kwa mustakabili wa taifa hili ikiwa hali hii itachukuliwa kirahisi ama kupuuzwa, kulindana kutokana na itikadi za vyama vya siasa au kwa maslahi binafsi.
Migogoro ya wafugaji na wakulima imeanza kitambo na wananchi  pamoja na wabunge hasa wa upinzani wamekuwa wakisema jambo hilo bungeni lakini Serikali imekuwa ikilichukulia ni propaganda zao za kujitafutia umaarufu.
Bila shaka maauji ya watu zaidi ya kumi yaliyotokea Wilaya ya Kiteto yamethihirisha na kuonyesha sura na uhalisia wa  kile kilichokuwa kikisemwa  mara kwa mara lakini kinachukuliwa poa.
Hakuna haja ya kuelezea kile kilichosemwa na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndungai mbele ya Waziri Mkuu Pinda alipotembela wananchi wa Kiteto, kwa kuwa alisema wazi baadhi ya viongozi wa Serikali wanashiriki kwa namna moja katika mauaji hayo kwa manufaa yao binafsi.
Wakati tunatafakari ya wafugaji na wakulima lakini inaonekana kuna mkakati wa ubaguzi na chuki  unaendeshwa chini chini na viongozi  katika sehemu za kazi kwa kuangalia itikadi za vyama vya siasa, mkakati huu unaweza kuwa hatari kwa ustawi wa taifa.
Ni hali ya kustajabisha kuona Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo akifanya kazi kwa ubaguzi na chuki kutokana na itikadi za vyama vya siasa.
Ubaguzi  na chuki wa mkuu huyo ulidhihirika January 17 mwaka huu  wakati wa hafla iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Taka Mwanza (MWAUWASA) ya kupokea hundi ya mkopo Sh milioni 300 kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (LAPF).
Fedha hizo zilitolewa na LAPF kwa ajili kukikopesha Chama cha Akiba na Mikopo cha Mamlaka ya Maji Safi na Taka Mwanza (MWAUWASA-SACCOS) ambacho imekuwa mkombozi wa watumishi wa mamlaka hiyo.
Katika hali ambayo haikutarajiwa wageni wa  LAPF waliokuwa wametoka Dodoma na watumishi wa Mwauwasa wakiwa tayari kumpokea mgeni rasmi ambaye ni Ndikilo, ilikuja taarifa kwa wote kwamba amepata dharura hivyo hatafika.
Kitendo hicho kiliwashangaza watu wengi  na kuhoji angemtuma hata mwakilishi wake kwa kuwa wageni walikuwa nje ya ukumbi wa Gand Hall kwa ajili ya mapokezi.
Macho ya wageni na waalikwa yalielekezwa kwenye ofisi ya Ndikilo ilipo kwa kuwa ni karibu kutoka eneo la hafla ilipokuwa ikifanyikia sawa na mita 95  huku kila mmoja akitafsiri ajuavyo juu ya kitendo hicho.
“Lakini wakati watu wakiondoka eneo hilo ilidokezwa  taarifa nyingine kwamba  Ndikilo hakuweza kufika kwa sababu Meneja  wa Saccos hiyo, Tungaraza Njugu  ni kada  na kiongozi mkubwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivyo hawawezi kukaa meza moja”.
Ilifafanuliwa kwamba Meneja Njugu  ambaye ni Kiongozi wa Operesheni Kanda ya Ziwa Magharibi wa Chadema amekuwa akimtukana Ndikilo katika majukwaa na mikutano ya  kisiasa juu ya utendaji wake, hivyo upande mmoja kuwa na  chuki.
MTANZANIA ilifunga safari kwenda ofisi ya Saccos ya Mwauwasa ili kujua kwa kina hali hiyo ambayo viongozi ambao ni waajiriwa wa Serikali kufikia hatua ya kufanya kazi kwa chuki kutokana na itikadi za kisiasa.
Njugu anaanza kwa kusema anasikitishwa na kitendo kilichotokea na kuongeza kwamba imedhihirisha Ndikilo anaongoza Mkoa wa Mwanza kwa itikadi ya kichama na ubaguzi wa kisiasa.
Anasema haamini kama Ndikilo ametumwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) au ndio sera ya chama hicho  katika kuongoza  kwa ubaguzi wa watumishi kwa mlengo wa itikadi za kisiasa.
Njugu anasema taarifa ya Ndikilo kushindwa kufika eneo tukio kutokana na yeye kuwa kada wa Chadema ilielezwa na Zacharia Membo ambaye ni Afisa Utumishi Mwauwasa.
Anasema hali hiyo imempa wasiwasi juu ya usalama wake, ajira na mambo mengineya kifamiia  kwa kuwa Ndikilo ana nafasi ya kumtendea kitu chochote kwani ni mkuu wa mkoa na Mwenyekiti wa kamati  ulinzi na usalama.
Njugu anasema imedhihirisha wazi watumishi wa Serikali ambao ni makada wa Chadema wapo katika hali ya kubaguliwa na inaonyesha hawana haki ya kazi au kuajiriwa serikalini.
Anasema alipata nafasi ya  meneja wa Saccos hiyo kutokana na elimu na utalaamu wake, hivyo kuwa kada wa Chadema si dhambi na kuongeza kwamba kamwe  hafanyi kazi kwa itikadi za kisiasa.

Njugu anasema kuna kila sababu ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko ya nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa kwani imedhihirisha chanzo cha madiwani watatu wa Chadema kufukuzwa ni nguvu yake inachangia.
“Sasa hivi Ndikilo namweka kama adui wangu namba moja katika maisha yangu, familia na ajira hivyo vyombo vya usalama nataka vijue hivyo nikipata tatizo lolote chanzo ni chuki za kisiasa za upande mmoja”.
Lakini anasema kutokana na ubaguzi huo na chuki wa Ndikilo haziwezi kuwa kikwazo katika kutekeleza majukumu yake ya kazi na kisiasa anakupokuwa nje ya Saccos.
Njugu anasema kwa nafasi yake hiyo hajawahi kufanya upendeleo wowote dhidi ya watumishi wa Mwauwasa na wengi wao wamejenga nyumba na kununua gari kupitia Saccos yao.
Inaonekana Ndikilo alikuwa na chuki dhidi ya mamlaka hiyo kwani aliwahi kulalamika mbele ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) juu ya tabia ya Mkurugenzi wa Mwauwasa, Anthony Sanga kushindwa kutoa taarifa kwake wakati Naibu Waziri wa Maji, Benilith Mahenge alipokuja Mwanza January 3 mwaka huu.
Ni kweli kabisa wakati Mahenge alipokuja kukabidhi vitendea kazi kwa halmashauri nne za Geita, Ukerewe, Sengerema na Nansio hakuwapo Mkuu wa mkoa wala askari yeyote kwa ajili ya ulinzi, hindicho ndicho kilimchomkasirisha na kuamua kumsema  Sanga mbele ya RCC.
Yamekuwapo na malalamiko dhidi ya Sanga kwamba ni miongoni mwa viongozi wababe, kiburi sawia na Ndikilo lakini wanaoumia kutokana na uhasama huo ni wananchi wanaohitaji huduma  za kijamii.
Mhandisi Sanga amekuwa akilalamikiwa na wananchi pamoja na waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza juu ya kauli zake na hata kuwatishia maisha pale wanapokuwa wakimbana kutaka taarifa ya Mwauwasa kutokana na malalamiko ya wananchi.
Hata wanapojaribu kuandika maswali na kuyakabidhi kwake amekuwa akiyapuuza lakini wanapojaribu kuandika hali halisi ndipo ugomvi unapotokea na kutoa vitisho.
Mmoja wa watumishi wa Mwauwasa ambaye hakutaka jina lake litajwe anasema ni dhahiri sasa kuna mkakati wa kumwondoa Njugu katika nafasi ya umeneja kwa kuwa elimu yake haikidhi viwango vya kusimamia saccos hiyo kwani imefikia kumiliki mabilioni ya fedha.
Ni wazi sasa  kumeibuka kasumba ya kutoelewana kati ya viongozi ngazi ya halmashauri, wilaya, mkoa na taasisi zake kutokana na itikadi za kisiasa na kusababisha kukwama kwa shughuli za maendeleo katika maeneo husika.
Itakumbukwa mwishoni mwa mwaka jana mpaka sasa kumekuwapo na migogoro kadha wa kadha maeneo mbalimbali  nchini kwa viongozi wa kulalamikiana huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuingilia majukumu ya mwenzake.
Pia kumekuwapo na hali ya kutofautiana kauli juu ya jambo moja  ambapo upande mmoja umekuwa ukidai kutenda haki huku mwingine ukilalamika.
Tumeshuhudia mkoani Arusha, mkuu wa mkoa huo akitofautiana kauli na Mkurugenzi wa jiji hilo juu ya wafanya biashara wadogo katikati ya jiji hilo na kusababisha madiwani kugawanyika katika pande mbili.
Ukiachia hilo kumekuwapo na mgogoro kati ya Meya wa Ilemela  na Mkuu wa wilaya mkoani Mwanza kwa kila mmoja kudai kuingilia majukumu ya mwingine.
Wimbi hilo linaonekana kuwagusa sana wakurugenzi wa Halmashauri kutofautiana na madiwani na watendaji wengi, kwa mfano Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hassan Hidda amekuwa katika mgogoro na madiwani jambo ambalo linakwamisha maendeleo.
Hiyo ni mifano michache ambayo inaonesha kuna wimbi la viongozi walioaminiwa na kupewa dhamana ya kuwatumikia wananchi kushindwa kushirikiana na kuanza kutuhumiana.
Kwa tukio la RC Ndikilo la kutohudhuria katika hafla hiyo zikiwa zimesalia dakika kama kumi lilionesha sura mbaya kwa wageni waliotoka Dodoma kwa ajili kutoa mkopo kwa Mwauwasa, mpaka sasa haijulikani wageni hao walipewa majibu gani.
Ni vema sasa Rais Kikwete akawatazama watu wake kwa namna nyingine katika nafasi walizopewa kuziongoza kwa kuwa wanaelekea kuleta mgawanyiko ndani ya jamii moja na taifa moja vingine itafikia hatua ya wafugaji na wakulima.
0683608958
MWISHO.






3 comments:

  1. hodi ni wewe katika haraka haja mkopo kulipia kuanza yako madeni ya kuanzisha biashara au nyumba ??? Kisha inakuja teksi kampuni una imani na relay juu ya 100% uhakika sababu hii ni kampuni ambapo i cashed mkopo wangu kwa mama yangu Stella dawa leo ili kuwasiliana na René Mikopo Firm halisi kupimwa na kuaminiwa na leo mimi nina furaha i got mkopo wangu wa $ 120,000 leo ili kupata kushikamana leo mrsstellareneloanfirm@hotmail.com} {barua pepe hapa chini na kupata jibu la matatizo yako yote kwa sababu Siwezi Kunyamaza ushuhuda huu mkubwa peke yangu binafsi ili i aliamua kuandika kwenye tovuti kwa sababu kula furaha kubwa kwa yangu moyo na leo mimi nina kuishi maisha mapya shukrani kwa wote Stella René


    kolochatechee


    ReplyDelete
  2. Ni wewe kuangalia kuanza mkopo biashara au kulipa
    Hesabu za
    Hiyo ni kwa nini tuko hapa kuwasaidia wenye
    Unahitaji mkopo
    kwa kiwango cha 3%
    wasiliana nasi leo kupitia barua pepe:
    joerichardloanfirm@gmail.com
    Biblia inasema: "" Luke 11:10 Kila mtu ambaye anauliza
    kupokea; atafutaye hupata; na kwamba
    makofi mlango wazi "kwa kamwe kuondoka
    wao miss nafasi kwa sababu Yesu ni
    yule jana, leo na hata milele
    zaidi.Tafadhali hizi ni nia mbaya na Mungu
    wakihofia watu. Wewe ni ushauri wa kujaza na kurudi
    .. Maelezo hapa chini name: __________
    ____________ Anuani yako: ____________________
    Nchi yako: ____________________ wake
    Kazi: Mikopo Kiasi __________________
    Inahitajika: ______________ Mikopo Muda: ______
    ______________ Mapato ya kila mwezi: __________________
    Kiini simu: ________________ Je,
    kutumika kwa ajili ya mkopo kabla ya: ________________
    haraka ndani na nje ya fedha dhiki, machafuko na
    ugumu kuwasiliana RichardLoan Corporation
    Leo email: joerichardloanfirm@gmail.com.you
    Utapata mkopo wako bila kuchelewa kuwa Apply.and
    heri

    ReplyDelete
  3. I am a veteran with the world trade organization humanitarian delivery agency, an ancillary of the UN..
    Mrs. Bernice Clark 69 died of covid-19 related virus. Before her death she left manifold amounts with a security & finance firm in Europe for preservation. she disclosed that the trust-funds should not be left unclaimed. You are to stand as the stipendiary to  late Bernice Clark.
    Get back to us with your interestedness at (wldtrdeorgnztionhumangcy@gmail.com). and contact data for all other formalities which are certifiable.
    Hoping to have an opulence pact with you on communal trust.

    ReplyDelete