Sunday, 25 August 2013
OPERESHENI YA KUONDOA POLISI WASIOFAA
Na Benjamin Masese, Dar es Salaam
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi ametembeza panga kali ndani ya Jeshi la Polisi na kuwafukuza kazi maofisa wanne huku baadhi yao wakivuliwa vyeo vyao.
Maofisa hao ni wale waliohusika kushiriki kwa namna moja au nyingine katika matukio yaliyotokea mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma na kulalamikiwa vikali na wananchi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Da r es Salaam jana alisema askari hao ni wale waliohusika kutumia gari la kutuliza Ghasia (FFU) kubeba bangi mkoani Arusha na Kilimanjaro
Tukio jingine ni lile la askari mkoani Morogoro kutumia fuvu la binadamu kumbambikizia mfanyabishara kwa lengo la kupata fedha, mauaji ya mfanyabishara wa Wilaya ya Kasulu yalifanywa na askari polisi.
Tukio la Bangi
Dk. Nchimbi alisema katika sakata la tukio la bangi amemvua madaraka yote aliyokuwa nayo Mkuu wa Kikosi cha FFU Mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi, Ramadhan Giro kwa kosa la kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maofisa walio chini yake na kusababisha kutoke tukio hilo.
Pia amemsimamisha kazi Ispekta Isaac Manoni na kushitakiwa kijeshi kwa kosa la kutumiwa kumtorosha mtuhumiwa ambaye ni polisi Edward Mwakabonga aliyekuwa dereva wa gari la FFU kitendo kilicholifedhehesha jeshi hilo.
“Katika tukio hilo kitendo cha Inspekta Salum Kingu wa kikosi cha FFU Mkoa wa Kilimanjaro kubaki kwenye gari mita 80 kutoka ilipo nyumba ya mtuhumiwa Edward alipopelekwa Moshi kukabishi vifaa vya jeshi letu kimechangia, hivyo tumempa onyo kali la kuwa makini na utendaji wake.
“Pia Inspekta Mikidadi Galilima kutotimiza wajibu wake ipasavyo katika kumshauri Mkuu wa FFU Mkoa wa Arusha juu ya ukaguzi na usimamizi wa rasilimali na kujaribu kuficha ukweli wa tukio, nimempa onyo kali Inspekta Galilima.
“Katika tukio hilo nimempandisha cheo ASP Francis Duma aliyekuwa kiongozi wa askari 14 katika kupambana kulikamata gari la FFU lililobeba bangi na kuwa Mrakibu wa Polisi,askari wengine 14 nimegiza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Said Mwema kuwapandisha vyeo kwa sababu wapo ngazi yake,”alisema.
Tukio la fuvu
Dk. Nchimbi alisema amewavua madaraka yote waliyonayo Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Mvomero, Inspekta Jamal Ramadhan na Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila, Inspekta Juma Mpamba kutokana na kuonyesha udhaifu mkubwa katika utendaji kazi wa kushindwa kuwasimamia askari wake na kushindwa kuwakamata matapeli na hawalifu ambao ni vinara.
Dk. Nchimbi alisema kabla ya tukio la askari watatu kushirikiana na raia wawili kumbambikizia fuvu la binadamu mfanyabishara Samson Mwita, Inspekta Ramadhan alikuwa na taarifa za mpango wa tukio hilo la askari wake kushirikiana na rai kufanya kufanya hivyo lakini hakumtaarifa Inspekta Mpamba.
Alisema askari wote waliohusika na tukio hilo ambao ni Sajeti Pasua Mohamed, Sajeti Sadick Madodo Koplo Nuran Msabaha wamefukuzwa kazi na kushitakiwa kwa uhalifu waliotenda sambamba na raia wawili ambao ni Rashid Hamisi na Adamu Peter.
Kupiga na kuua raia
Dk. Nchimbi alisema Disemba 25 mwaka jana askari wa kituo kidogo cha polisi cha Heru Ushingo kilichopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa pamoja walimpiga raia ambaye ni marehemu sasa Gasper Sigwavumba na kumweka mahabusu bila msaada wowote wa matibabu.
Alisema katika tukio marehemu alipasuka bandama kutokana na kipigo hicho na kuongeza kwamba upelelezi mbovu uliofanywa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu, ASP Daniel Bendarugaho kesi ya mauaji iliweza kuondolewa mahakamani.
Dk. Nchimbi alisema wakati kesi inaondolewa mahakamani askari waliohusika ambao ni Koplo Abraham Peter na PC Simon Sunday walikuwa wamefukuzwa kazi na kuwa huru jambo ambalo lilizua malalamiko.
“Kutokana na ASP Bendarugaho kutokuwa makini katika kusimamia upelelezi wa jalada husika la kesi hiyo ya mauaji tunavua madaraka na upelelezi unaanza upya ili haki itendeke,”alisema.
“Operesheni ya kulisafisha jeshi hilo itaendelea hadi litakapokuwa safi, leo hii wananchi wamekata tama kabisa na jeshi la polisi ukimwambia kitu chochote juu ya polisi haamini.
“Kwa kipindi nitakachokuwa naongoza wizara hii, nitalisafisha na Watanzania watarudisha imani kwa polisi, katika matukio haya matatu askari waliohusika moja kwa moja wamefukuzwa kazi na kushitakiwa.
“Haya ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa na timu niliyoiunda ambapo Mwenyekiti wake alikuwa Mkurugnezi Mkuu wa Idara ya masuala ya Malalamiko Makao Makuu, Augostine Shio.
BOMBA LA GESI KUTANDAZWA LEO.26/8/2013
Bomba la gesi ya Mtwara kutandazwa leo
Na Benjamin Masese, aliyekuwa Lindi
BOMBA la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam,
linaanza kutandazwa leo likianzia mkoani Lindi.
Kutokana na hali hiyo, Serikali imeonya kwamba,
yeyote atakayethubutu kuharibu miundombinu ya bomba hilo, atachukuliwa hatua.
Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alipofanya ziara ya kukagua, ubora wa vifaa, rasilimali
watu na maandalizi ya miundombinu ya
kutandaza bomba hilo.
Wakati wa ziara hiyo ya siku moja, alikuwapo pia Balozi
wa China nchini, Lu Youging, viongozi mbalimbali wa Serikali na viongozi wa kampuni
zinazotandaza bomba hilo.
Profesa Muhongo alisema ameridhishwa na maandalizi
yanavyokwenda, kwa kuwa kuna vifaa vya kisasa na imara.
Kesho kutwa (leo), utandazaji wa bomba unaanza rasmi
na kwa maandalizi niliyoshuhudia, nina imani mradi huu utakamilika kabla ya Desemba
mwaka 2014.
“Naomba Watanzania wawe na imani kubwa na watoe ushirikiano
kwani utandazaji wa bomba utafanyika katika pande zote mbili, kwa maana ya nchi
kavu na baharini.
“Mradi huu ni wa gharama kubwa na kama mnakumbuka,
tulikopa fedha kutoka Benki ya Exim ambazo ni Dola za Marekani bilioni 1.2 kwa
masharti nafuu.
“Pamoja na kwamba nia yetu ni nzuri, kuna baadhi ya
watu wasiopenda maendeleo ya nchi hii, nataka kuwahakikishia Watanzania wote,
kwamba usalama wa miundombinu hii utakuwa shwari na kama mtu anataka
kushughulikiwa na Serikali, basi ajaribu kuihujumu atakiona cha mtema kuni.
“Hapa tumeshuhudia Watanzania 45 walioanza kupata
ajira kama madereva, vibarua, kampuni za usafirishaji, huu ni mwanzo tu na ikifika
sehemu ya kuhitaji watu wenye utaalamu, wataajiriwa wenye utaalamu,” alisema
Profesa Muhongo.
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, mabomba yanayotandazwa
ni ya aina mbili yakiwamo ya inchi 36 na uzito wa tani tano na yenye inchi 24 yakiwa
na tani tatu ambayo alisema kwa ujumla wake yatadumu kwa miaka 30 na kama
yakitunzwa vizuri yatadumu hadi miaka 70.
“Tunataka ifikapo mwaka 2016, tuwe na umeme wa
megawati 3000 na mwingine wa ziada wa utakaokuwa ukiuzwa nje ya nchi ikiwamo Kenya
ambayo imeleta maombi ya kuuziwa megawati 1000,” alisema.
Pamoja na kufanya ziara hiyo juzi, Profesa Muhongo
alisema itakuwa ni endelevu na itakuwa ikihusisha waandishi wa habari.
Naye, Balozi Youging, alisema gesi ni kitega uchumi kizuri
ambacho kinaweza kuwaondoa Watanzania katika umasikini.
“China ni moja ya nchi iliyonufaika na gesi na ndio
maana raia wake ni wataalamu wa nishati hiyo, naamini upatikanaji wa gesi hapa
Tanzania, utasaidia Watanzania kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni.
Kwa upande wake, Meneja Mradi wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania, Mhandisi Baltazari Thomas, alisema hadi sasa
watu 163 wamepata ajira katika awamu ya
kwanza na kati ya hao Watanzania ni 68.
Mwisho.
Rufaa dhidi ya Zombe kusikilizwa leoNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam
MAOMBI ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ya kuongezewa muda wa kukata rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na askari wenzake wanane walioachiwa huru katika shtaka la mauaji, yanatarajiwa kusikilizwa leo.
Maombi hayo yanatarajiwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Aloyisius Mujuluzi.
Katika shauri hili, DPP aliwasilisha maombi ya kuomba kuongezewa muda wa kukata rufaa, baada ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, kutupilia mbali rufaa ya awali kwa sababu ilikuwa na makosa ya kisheria.
Rufaa hiyo ilitupwa baada ya kubaini kuwapo kwa dosari katika hati ya kusudio la kukata rufaa na mahakama kukataa kuamuru makosa yaliyojitokeza yafanyiwe marekebisho.
“Kusudio la kukata rufaa ndio linatengeneza rufaa yenyewe, kwa kuwa kuna makosa, hakuna rufaa iliyopo mahakamani, kama makosa yangejitokeza katika rufaa yenyewe, Mahakama ingeweza kutoa maelekezo ya kufanyiwa marekebisho, rufaa inatupwa, Jamhuri ina haki ya kuwasilisha rufaa nyingine nje ya muda, baada ya kuomba kufanya hivyo,” alisema Mwenyekiti wa Jopo la Majaji Watatu, Edward Rutakangwa.
Majaji wengine waliokuwa wakisikiliza rufaa hiyo kabla ya kutupwa ni Jaji Mbarouk Mbarouk na Bethuel Mmila ambao awali walipoketi kwa ajili ya kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na DPP kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ziliibuka hoja za dosari katika hati ya kusudio la kukata rufaa.
Zombe na wenzake walikuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini wakazi wa Mahenge Morogoro pamoja na dereva teksi mmoja.
Kabla ya jopo la mawakili wa Serikali lililokuwa linamwakilisha DPP ambao ni Mawakili wa Serikali Wakuu, Edwin Kakolaki, Vitalis Timon, Prudence Rweyongeza na Mawakili Revocatus Mtaki na Alexander Mzikila, halijaanza kuwasilisha hoja zao za kukata rufani, Jaji Mbaraouk alilihoji jopo hilo kuhusu dosari hiyo.
“Mahakama inataka kujiridhisha juu ya kinachosomeka katika hati ya kusudio la kukata rufaa, ambayo inasema mnapinga hukumu iliyotolewa na Jaji Massati wa Mahakama ya Rufaa. Sasa hii inakuja kwetu kama marejeo au mapitio," alihoji Jaji Mbarouk.
Hata hivyo, Wakili Timon, alikiri kuhusu dosari hiyo na hivyo kuiomba Mahakama kuwaruhusu kufanya marekebisho na kisha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo.
Jaji Rutakangwa alihoji upande wa Jamhuri kuwa hati hiyo ina dosari, kwa kuwa inaonyesha wanakata rufaa kupinga hukumu ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa, wakati hajawahi kukaa kusikiliza shauri hilo kwa kuwa si sahihi.
Ombi la mawakili wa Serikali la kuomba kufanyia marekebisho hati hiyo, lilipingwa vikali na mawakili wanaowawakilisha Zombe na wenzake ambao ni Richard Rweyongeza, Majura Magafu na Dennis Msafiri.
Katika shauri hili, mbali na Zombe, wajibu rufani wengine ni polisi Christopher Bageni, Ahmed Makele, Jane Andrew, Koplo Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abeneth Saro, Rajabu Bakari na Festus Gwasab.
Serikali ilikata rufaa hiyo kupinga hukumu iliyotolewa Agosti 17, 2008 na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
mwisho.
Nyavu haramu za Sh milioni 150
zateketezwa
Na Ahmed
Makongo, Bunda
NYAVU haramu 3,280 zenye thamani ya
zaidi ya Sh milioni 150, zimekamatwa wilayani Bunda, mkoani Mara na kuteketezwa
kwa moto.
Nyavu hizo ziliteketezwa jana kwa
usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo,
Mirumbe alisema kuwa nyavu hizo ambazo ni pamoja na makokolo ya kuvulia
sangara, nyavu zenye matundu madogo, timba na makokolo ya dagaa, zimekamatwa na
vyombo vya dola kutokana na msako unaoendelea wilayani hapa.
Alisema kuwa msako huo unashirikisha
askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), polisi, mgambo pamoja na maofisa wa
idara ya uvuvi.
Alisema operesheni hiyo aliianzisha
mwenyewe na kwamba itakuwa endelevu kwa kuwa lengo lake ni kutokomeza wavuvi
haramu wilayani hapa.
Ili kuhakikisha uvuvi haramu
unakomeshwa wilayani hapa, aliwataka viongozi wa Serikali za vijiji, kata na Vikundi
vya Ulinzi wa Rasilimali za Ziwa Victoria (BMU), kuhakikisha wavuvi haramu
wanakamatwa.
Alisema kama uvuvi haramu utaendelea
katika baadhi ya maeneo, kitakachofuata ni kukamatwa kwa viongozi wa maeneo utakakokuwa
ukifanyika uvuvi huo.
“Hatua ifuatayo ni kukamata viongozi
wa Serikali za vijiji na kata na wale wa BMU ambao tutakuta kwenye maeneo yao
kunaendeshwa shughuli za uvuvi haramu,” alisema Mirumbe.
Aliwaonya viongozi hao kutojihusisha
na shughuli za uvuvi haramu, kwa kuwa inasemekana baadhi yao wanafadhili wavuvi
hao.
Naye, Ofisa Uvuvi wa Wilaya ya
Bunda, Stephen Ochieng, alisema nyavu hizo zilikamatwa katika Tarafa za
Kenkombo na Nansimo ambako ndiko uvuvi haramu ulikoota mizizi.
Aliongeza kwamba, wapo wavuvi haramu
ambao wamekuwa wakitumia sumu na kwamba uvuvi huo unahatarisha afya za wananchi
pamoja na kuua viumbe hai wa majini.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba
viongozi wa wilaya jirani zilizoko kwenye ziwa Victoria, kudhibiti wavuvi
haramu, kwani unapofanyika msako katika Wilaya ya Bunda, baadhi ya wavuvi hao hukimbilia
katika wilaya hizo.
Mwisho.
Thursday, 15 August 2013
LWAKATARE HOI
Polisi, Dk. Slaa jino kwa jino
Na Benjamin Masese, Dar es Salaam
WAKATI Jeshi la Polisi likiendelea kumng’ang’ania Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare kwa tuhuma za kupanga njama za kudhuru watu, imedaiwa kuwa afya ya kiongozi huyo imezidi kudhoofika.
Na Benjamin Masese, Dar es Salaam
WAKATI Jeshi la Polisi likiendelea kumng’ang’ania Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare kwa tuhuma za kupanga njama za kudhuru watu, imedaiwa kuwa afya ya kiongozi huyo imezidi kudhoofika.
Tuesday, 13 August 2013
TUJADILIANE LEO
Hivi kulingana na matukio haya yanayotokea ya ukatili kwa raia, wizi, utekaji na masuala kama hayo yanaashiria nini? tujadili, tafadhali unapochangia hapa toa hoja sio kushambulia mtu kwa itikadi na dini zako.
UKATILI HUU MPAKA LINI TANZANIA?
![]() |
Mama akipigwa na mume wake baada ya kutofautina |
![]() |
Baba akimdhibiti mke wake kwa kumkata mapanga baada ya kuona ngumi, mateke na fimbo havikutosha |
Na Benjamin Masese, Dar es Salaam
UKATILI wa kijinsia ni jambo
kubwa kwenye ajenda za haki za binadamu
kimataifa.Ukatili unaweza kuwapata wanaume na wanawake lakini mara nyingi
wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa.
Hali hii imetokana na mifumo mbalimbali iliyopo na uhusiano wa
kijinsia ulivyo katika jamii zetu hapa nchini ambapo kundo moja hujiona ni bora
kuliko kundi lingine.
Kwa miaka mingi wanaume
wamechukuliwa kuwa katika daraja la juu kuliko mwanamke nah ii imejionyesha na
kuendelea kuonekana wazi katika nyanja
zote za kijamii, kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi.
Mazoea hayo yamejengwa tangu
zamani huku kukiwa na ngazi za kifamilia hadi kitaifa jambo ambalo ni hatari
katika jamii nyingi Barani Afrika na sehemu nyingine duniani.
Kutokana na hali hiyoilivyo
mpaka sasa, kuna haja kubwa ya kutoa elimu juu ya ukatili katika jamii zetu
hususani vijijini kunakotokea kila siku vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.
Bila Serikali, taasisi,
mashirika na wadau wengine wanapaswa kuungana pamoja na ili kuwaelimisha jamii
juu ya kupambana na kuzuia ukatili wa kijinsia ili kuleta mabadiliko katika
jamii.
Sote tunatambua kwamba
ukatili ni kitendo chochote anachofanyiwa binadamu na kumsababishia maumivu au
athari kimwili, kiakili au kisaikolojia.Kumekuwapo na vitendo vya ukatili vingi
tena vya kukusudia, kulazimisha, kutisha au kugofya dhidi ya wanawake kutaka
kufanya jambo au tendo la ngono bila hiari yao.
Binadamu yeyote anaweza
kufanyiwa ukatili wa aina tano
ukitegemea na utamaduni na
historia ya jamii husika. Mara nyingi
ukatili huo hufanyika kati ya wanandoa wa wapenzi lakini wanawake mara nyingi
wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na ukatili wa kijinsia katika uhusianohuo.
Moja ya ukatili ni ule wa
kimwili ambao mtu hufanyiwa kitendo ambacho kinaumiza mwili na madhara yake
huonekana moja kwa moja na wakati
mwingine mtendewa ukatili anaweza kuhisi maumivu bila mtu mwingine kutambua
kuwa amefanyiwa ukatili wa kimwili.
Baadhi ya mifano ya ukatili
wa kimwili ni pamoja na vipigo, shambulio la kimwili, kuchomwa moto, matumizi
ya silaha, kuvutwa nywele, kusukuma, kunyonga mkono au mguu, kupigwa kichwani
na kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu yoyote ya mwili.
Pia upo ukatili wa kisaikolojia ambao mtu
anatendewa na unamsababishia maumivu
kiakili, kihisia huku mtenda kutotambua mwenzake anaathirika, mfano matusi kwa
njia ya maneno au ishara yenye lengo la kudhalilisha, vitisho na kutishia
kufanya fujo, maneno ya kufehedhesha, kudharau, kutishia kutoa siri, kuingiliwa
faragha, kutishiwa kuuawa na mengine mengi.
Vile vile kuna ukatili wa
uhusiano wa kingono ambao huambatana na
vitendo vinavyohusiana na masuala ya ngono, kwa mfano unyanyasaji wa kijinsia,
kujamiiana kwa maharimu, ubakaji ndani ya ndoa, ulawiti, utekaji na
usafirishaji wa wanawake au wanaume na
watoto kwa ajili ya ngono na vitendo vingine vya namna hiyo.
Upo ukatili wa kiuchumi ambao
humnyima fursa za kiuchumi mwanamke au mwanaume katika kujiongezea kipato na
kuchangia katika maendeleo.Aina hiyo ya
ukatili huwapata wanawake kutokana na hali yao ya kuwa tegemezi kwa wenzi wao.
Kitendo cha wanawake kuwa
tegemezi kwa wanaume kimekua kinawaathiri sana
kwani wanakosa kauli katika mali
za familia na kutoshirikishwa kwenye maamuzi ya maendeleo.
Pia kuna ukatili unaotokana
na tamaduni au mila potofu zetu hapa nchini ambazo zinakinzani na haki za
binadamu jambo linalochangia kuwapo kwa vitendo vya ukatili. Baadhi ya ukatili
wa mila potofu ni pamoja na ndoa za kushurutisha za utotoni, kutakasa wajane,
kurithi wajane, utekeaji, matambiko ya kingono kwa watoto, miiko ya chakula na
ukatili utokanao na mahari.
Kutokana na uendelezaji wa vitendo vya ukatili nchini,
kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake
Tanzania (WLAC) kimeamua kuanzisha
kampeni ya kupinga vitendo hivyo na kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake ili kuleta usawa wa kijinsia Tanzania.
Taasisi ya WLAC ni shirika lisilo la Serikali lililoanzishwa
mwaka 1994 chini ya sheria ya makampuni sura ya 212 na pia limekuwa
likiendeleza shughuli za kitengo cha
msaada wa sheria SUWATA kilichoanzishwa
mwaka 1989.
Kati ya madhumuni ya WLAC ni
kutoa msaada wa sheria ju ya masuala yanayowakabili wanawake kama
ndoa, mirathi, mikataba, biashara, ajira, uwakilishi mahakamani na huduma
nyingine zinazofanana na hizo.
Pia imekuwa katika harakati
za kujenga mtandao wa mashirika pamoja na taasisi zenye mwelekeo unaofanana na
WLAC na kuratibu kwa pamoja shughuli za uhamasishaji umma kuhusu haki za
wanawake na watoto.
Si jambo la kificho kwani
wanawake wamekuwa katika changamoto kubwa hasa pale wanapokuwa katika ajira
rasmi na hata zisizokuwa rasmi, baadhi yao
wamekuwa wakikosa nafasi za kufanya kazi
mahali walipoomba kazi auhata katika ngazi ya familia kutokanana sababu
mbalimbali.
Katika maeneo ya kazi, uzoefu
unaonyesha wazi kuna kazi za wanawake na kazi za wanawake, wanawake
waliobahatika kupata ajira wengi utawakuta nafsi za chini zaidi kama mapokezi, uhudumu wa ofisi, kazi za usafi na katibu
mukhatsi.
Wakati mwingine baadhi ya
wanawake wamelazimika kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na wakuu wao wa kazi
ili kupata mahitaji yao.Wanawake wa namna hiyo huishia kwenye migogoro na waume
zao au wapenzi wan a hatimaye uhusiano huo huharibika kabisa na kufukuzwa kazi.
Kazi zinazohitaji mwanamke
kusafiri sana,
kufanya kazi muda mrefu, wakati wa usikuau zinazohusisha kukutana na watu
mbalimbali mara nyingi zimesababisha migogoro katika ndoa.
Hata hivyo wanawake wengi
wamekosa fursa ya kujishughulisha ili kuongeza pato la familia, ambapo kwa wale
waliobahatika kupata ajira zisizo rasmi wengi wao wanaishi kwa masharti na
kutokuwa huru na wanapata mapato yanatokanayo nakazi wanayofanya.
Suala la ukatili lina upana
wake ambapo upo ukatili wa kijinsia unaotokana na lugha ambapo maneno
mbalimbali yamekuwa yakitumika kumwelezea mwanamke ambayo uhalisia wake ni
ukatili wa kijinsia.
Maneno hayo yamekuwa
yakitolewa katika kuelezea maumbile na tabia ya baadhi ya wanawake, matumizi ya
lugha hiyo kwa sehemu kubwa huchangia kuonyesha mfumo dume ambao ndio
unaotawala maisha ya watu ya kila siku. Matumizi ya lugha yanadhihirisha dhana
potofu kwamba kundi la wanaume lina nguvu na ni bora kuliko wanawake.
Asilimia kubwa na mazoea
yaliyopo sasa ni kwamba neno mwanamke amekuwa akichukuliwa ni kama chombo cha
kumstarehesha mwanaume, mfano kuna maneno ya kama
changundoa, sahani ya babu, namba nane, twiga na mengine kam hayo ambayo
huonesha kuwa mwanamke ni dhaifu kuliko mwanaume.
Maneno mengine yanayoendana
na hayo wakati mwingine yanaweza kutolewa dhidi ya wanaume, kwa mfano bushoke,
dume la mbegu lakini yote yameelekzwa kwa wanawake kumuonyesha mwanaume ni
bora.
Hata hivyo upo ukatili katika
vyombo vya habari na matangazo ya kibiashara, mfumo wa habari na utoaji wa
habari zenyewe umekuwa ukionesha taswira ya mwanamke kama chombo cha
kumburudisha mwanaume, mfano matangazo, picha na mziki hutumiwa na kuonyesha
wanawake kama sehemu ya matangazo ya biashara.
Kutokana na hali hiyo hivi
karibuni WLAC kupitia wanasheria wake waliandaa semina iliyohusisha wanawake na wanaume wanaojiita wanabadiliko kutoka mikoa ya Dar
es Salaam na Pwani na kutoa elimu juu ya mambo kadhaa ya ukatili wa kijinsia
nchini unaotokea katika nyanja mbalimbali ndani ya jamii.
Wanasheria wa WLAC waliokuwa
wanatoa elimu kwa wanabadiliko ni pamoja na Lilian Lwanga na Hildegard Msina
ambao walitoa ushahidi jinsi wanawake wanavyoteseka ndani ya ndoa zao pamoja na
kunyang’anywa urithi wa mme wake mara anapofariki na kuacha familia.
Kwa upande Lwanga alibainisha
kwamba katika utafiti walioufanya katika kadhaa nchini wamebaini asilimia 75 ya wananawake walio ndani ya ndoa hawana
uhuru wa kijitawala katika maisha yao
ya kila siku kutokana na kufanyiwa vitendo vya ukatili na wenzi wao.
Pia anasema walibaini wanaume
wengi vijijini wamekuwa wakivunja ndoa zao au kuwatelekeza wake wao baada ya
kujifungua watoto wenye vichwa vikubwa, midomo ya sungura na wengine wa namna ambapo
aliitaka Serikali kuchukuliwa hatua za kisheria ili kukomesha hali ya ubaguzi,
unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake.
WLAC imeamua kuendesha
kampeni maalum ijulikanayo kwa jina la TUNAWEZA
kwa wanamabadiliko ili kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji nchini
ambavyo vinaonekanakuwa jambo la kawaida katika jinsia ya kike.
Lwanga anasema msaada wa kisheria unaotolewa
na WLAC umekuwa na mafanikio makubwa
kwani umeweza kuwasaidia wanawake kwa kuwawakilisha makahamani hadi kurudishiwa nyumba walizokuwa wamenyang’anywa
na ndugu wa marehemu kama urithi.
Anasema katika utafti wao
mikoani wamebaini wanawake bado wananyanyaswa, wanapigwa na waume lakini hawako tayari kuwasema kwenye vyombo vya dola
na kuongeza wameshuhudia ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya mtoto kuzaliwa
na kichwa kikubwa au mdomo wa wazi yaani wa sungura.
Lwanga anasema tatizo la
watoto kukimbilia mjini na kuwa kuombaomba linatokana na ndoa kuvunjika, elimu ndogo
kwa akina mama ya kutojua sheria zinazowapa haki yao, umasikini na mila potofu.
Anasema asilimia kubwa ya
wananchi hasa wa vijini wanaishi kwa kuzingatia mila zao, hawajui mabadiliko yaliyopo, wananyanyaswa kwa njia
ya ngono, kiuchumi, kishambulio na kisaikolojia lakini hawajui namna ya
kujisaidia kisheria kwani tangu awali Serikali haijaweka misingi ya kuwalinda
wananwake na kuwapa uhuru.
Pamoja na mambo mengi ya
unyanyasaji wa wanawake, Lwanga anaitaka Serikali kuacha mazoea ya kutegemea
asasi, mashirika na ufadhili wa mataifa makubwa ya nje kuja nchini kutatua
matatizo yanayowakabili wananchi wake badala yake inapaswa kupeleka elimu
vijijini hususani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Lwanga anasema kwamba ukatili
unaofanywa dhidi ya wanawake nchini hauwezi kuvumiliwa ambapo anawataka wanawake kuwafikisha wanaume kwenye vyombo
vya dola aple wanapotendewa vitendo vya unyanyasaji.
Anasema binadamu yeyote
anapofanyiwa ukatili humsababishia kuwa
na maumivu au athari kimwili, kiakili na kisaikolojia ambapo mwanamke anapofanyiwa
ukatili huo athari kubwa kuliko mwanaume.
Anasema hivi sasa WLAC kwa
kushirikiana na wakuu wa utekelezaji wa kampeni ya TUNAWEZA wamedhamiria
kufikisha elimu ya ukatili wa kijinsia kwa watu 1,600,000 ifikapo mwaka
2013 ikiwa lengo ni kupunguza vitendo hivyo kwa wanawake ambavyo vimeonekana
ndani ya jamii ni vitu vya kawaida.
Lwanga anasema madhumuni ya
WLAC ni kutoa msaada wa sheria juu ya masuala yanayowakabili wanawake kama ndoa, mirathi, mikataba, kusimamia kesi mahakamani,
kuendesha semina, ziara za mafunzo na kuhamasisha umma kuhusu haki za wanawake
na watoto.
Pamoja na mambo mengi , wanasheria
wa WLAC waliahidi kuendelea kutoa msaada wa kisheria mikaoni bure kwa wanawake
na watoto ikiwa lengo ni kuleta usawa wa kijinsia Tanzania.
Hivyo sasa wakati umefika kwa
Seriakli kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha vitendo vya unyanyasaji
kijinsia vinakomeshwa haraka, pia vitendo vilivyoibuka hivi karibuni vya mateka
kwa watu wanaopigania haki zao havipaswi kufumbiwa macho.
Tunapaswa kutambua kwamba
katika hali halisi binadamu wote wamezaliwa huru huru na wote ni sawa mbele ya
sheria hivyo hakuna mwenye haki ya kumfanyia mwenziwe ukatili wa aina yoyote.
Vitendo hivi vinapofanyika ni
kinyume cha sheria na mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ambayo Tanzania
imekuwa ikiisaini ili kushirikiana na mataifa makubwa kupambana na vitendo
hivyo, sasa ni mwito kwa serikali kutekeleza mikataba hiyo kwa vitendo na sio
maneno tupu. Maoni benjaminmasese@yahoo.com,
0655/0769-688300
MWISHOOO
Wakina mama wa kabila la Wangoreme wakifurahi wakati wa sherehe
Kabila la wangoreme na wakurya mkoani Mara wanavyokuwa wakisherekea shehehe za, harusi, kutahiriwa au kukeketwa. (chanzo. BBC Swahili)
|
DAR CITY 2013
Monday, 12 August 2013
SERENGETI ILIVYOVAMIWA VIJIJI VYAKE
HISTORIA YA WANGOREME
Na Benjamin Masese, Dar es Salaam
MKOA wa Mara ni miongoni mikoa ya Tanzania Bara ambapo mji wa Musoma ndipo makaoa makuu ya mkoa huo.
Mara imepakana na mikoa ya Mwanza na Shinyanga upande wa Kusini, Arusha upande wa Kusini-Mashariki, Kagera upande wa Magharibi mwa Ziwa Nyanza au Viktoria na Kenya upande wa mashariki.
Idadi ya wakazi ni zaidi ya milioni mbili na makabila ni mengi kuliko mikoa yote ya Tanzania ispokuwa Jiji la Dar es Salaam.
Baadhi ya makabila
yaliyopo Mkoa wa Mara ni wajaruo, wajita, waruri, wazanaki, wakabwa, wakiroba,
wasimbati, wangoreme, wakwaya, waikoma, wanata, waisenye, waikizu, wasizaki,
wasukuma, wataturu ne mengine wengi.
Kuna wilaya
ya saba ambazo ni Bunda, Serengeti, Tarime, Rorya, Butiama, Musoma Mjini na
Musoma Vijijini.
Katika
makala ya leo nitazungumzia kabila wa Wangoreme
wanaoishi Wilaya ya Serengeti. Wangoreme wametokea Carogos nchini Ghana miaka
mingi iliyopita.
Kabila la
Wangoreme na Waikoma mzazi wao ni mmoja
aliyejulikana kwa jina la Sabayaya Wandira ambaye ni miongoni mwa msafara wa
mtandao uliokuwa ukitoka Misri kupitia Somalia hadi Kenye ambapo waliingilia
Mto Mara na kuweka makazi yao Serengeti.
Msafara
mwingine wa kabila wa Wangoreme iliingia Serengeti kupitia njia ya Mkoa wa
Manyara na baadhi yao kuweka makazi yao hapo.
Vijiji vya
kabila la Wangoreme vilivyoitengeneza Wilaya ya Serengeti ni Mugumu,Ikorongo, Borenga, Nyiboko,
Buchanchari, Nyansurumunti, Mto Mara (Ghitende), Wigero, Baranga, Sirori Simba,
Remng’orori , Mikomariro.
Vingine ni
Mto Msamo-Tirina, Manchemwero, Nyankomogo, Issenye, Rigicha, Wegete, Nata,
Rubana na kuunganisha tena Mugumu ambapo ndipo makao Makuu ya Wilaya ya
Serengeti.
Lakini
Vijiji hivyo vimevamiwa na kabila la
Wakurya wenye asili koo ya waasi kwa upande Magharibi, upande wa Kusini
pamevamiwa na Waikizu na Waisenye na upande wa Magharibi wamevamia wakurya
halisi kutoka Kenye na Tarime.
Pamoja na
uvamizi huo lakini kabila la Wangoreme wameungana na kabila la Waikizu, Wanata
na Waisenye na kuwa kitu kimoja tofauti na Wakurya wenye tabia tofauti ya
ukatili na wizi wa mifugo.
Miiko ya Wangoreme
Mtu aliyeua mwenzake- Kabila la Wangoreme wamekuwa na miiko
yao kulingana na tukio lenyewe, kwa mfano mtu aliyeua mwenzake ukiachia masuala
ya kisheria, mara nyingi ukoo wa pande zote mbili hukaa na kukubaliana fidia
ambayo ni idadi ya ng’ombe kuanzia saba na mbuzi au kondoo saba.
Baada ya
fidia hiyo hufanyika matambiko fulani ambayo huashiria kusameheana na kushiriki kula chakula pamoja.
Mwanamke aliyeshindwa kujifungua- Mwanamke aliyeshindwa kujifungua
mtoto akiwa ndani ya ndoa au nje ya ndoa (ukiacha masuala ya kiafya), mara
nyingi huadhibiwa kwa kupakwa majivu kama mchawi.
Mbali ya
majivu hayo hunyolewa nywele kwa kutumia aidha chupa, wembe,mkasi na kisu huku
akikatwa au kung’atwa kichwani na
kufanyiwa vidonda vya makusudi, pia huanza kufanya kazi kabla ya kupona.
Kuoa-Katika suala la kuoa au kuolewa mara
nyingi wazazi wa kijana ndio wanaochagua
binti wa kuoa wakati upande wa binti wazazi hufuatilia historia ya jina na
wazazi wao kama wana sifa ya kuwa ndugu wa kuoana.
Idadi halisi
wanawake wa kuona ni kuanzia wawili hadi wadi wanne inategemea utajiri wa mtu
mwenyewe na wingi wa shughuli zake.
Baada ya
kuoana, marafiki wa pande zote mbili walisiosimamia ndoa hiyo hufanyiwa
matambiko ya kupakwa mafuta ya ng’ombe usomi
ikiwa ni laana ya kutoibiana wala
kutembea na mke wa mwenzie.
Mahali za kuoa mwanamke enzi za mababu zetu
ilikuwa ni ng’ombe 80-60, enzi za baba zetu 50-30 lakini hadi sasa 20-6 ambapo thamani ya ng’ombe mmoja sasa ni
Sh 300,000- 500,000.
Wanawake
kuoana ‘nyumba ntobhu’
Suala la
wanawake kuoana ni jambo ambalo linafanywa na Kabila la Wangoreme na Wakurya,
hii hufanyika pale aidha mwanamke anapojifungua watoto wote wa kike na kuolewa
wote.
Pia hutokea
pale mwana mke anapokuwa ndani ya ndoa lakini haukufanikiwa kupata mtoto hata mmoja ambapo hulazimika kuoa mke
mwenzake na kumpa uhuru wa kuzaa na mtu yeyote au kumchagulia mwanaume ndani ya
familia au ukoo wake.
Lengo kuu la
mke kuoa mke mwenzake ni kupata mtoto wa kiume ili kuendeleza ukoo wake na
kusimamia mali zake alizonazo.
Hukumu ya Wangoreme-Ukiweka pembeni sheria, hukumu kubwa ya Wangoremaikiwa
umefanya kosa kisha unakana kukusanywa
vitu vinavyoaminiwa ni hatari kwa afya yako na kulazimishwa kuviruka, pia kuna
fuvu la kichwa cha binadamu ‘ekehore’ ambalo huwekwa maji machafu ya nguo zako
na kunyweshwa.
Kukeketwa/kutahiriwa-Enzi za mababu wetu kijana au binti
kutahiriwa-kukeketwa ni miaka 18-25 kwa kutumia kisu na wembe lakini kutokan na
mabadiliko ya teknolojia jinsia ya kike imepigwa marufuku.
Pamoja na
kupigwa marufuku bado ukeketaji unaendelea kwa jinsia ya kike na vitendo hivyo
hufanyika kati ya umri mwaka mmoja hadi mitano kwani imani ni kupunguza hamu ya
kujamiliana. Pia Wangoreme wanaamini kuoa mwanamke ambaye hajakekeketwa ni
kuleta mkosi au haramu nyumbani.
Mapigano ya ukoo-Awali kulikuwa na mapigano ya koo na
koo ambapo yalimalizwa kabisa kwa kuanzisha utaratibu kubadilisha watoto katika
pande mbili jambo hilo husimamiwa na mabalozi wa nyumba kumi.
Ni kwamba
kama mwanamke amejifungua watoto zaidi ya watatu anachukuliwa na kukabidhiwa
koo nyingine hivyo upande wa pili kitendo ambacho kimewafanya kuwa kitu kimoja
yaani ndugu wa damu.
Chakula,ufugaji-Asili ya Wangoreme ni wafugaji wa
wanyama aina ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku na ndege aina ya kuku, bata, njiwa
ambapo viumbe hivyo hutumika kama kitoweo, kitega uchumi.
Pia mazao
yanayolimwa na Wangoreme ni mahindi, mtama, mihogo, viazi vitamu, maboga, ulezi
ambapo zao kuu la biashara ni pamba,
ufuta, karanga na Tumbaku.
Mboga halisi
ya Wangoreme ni majani ya kunde,maharage, mlenda, msusa, mchicha na wakati wa
kubadilisha au kuwapo kwa mgeni ni dagaa, nyama, samaki na vitoweo vingine.
Masharti katika Chakula.
Miiko ya
wangoreme ni kwamba wamefanya mgawanyo katika suala la nyama, kwanza vijana
wametengewa kula kidali, wanawake wametengewa kula shingo, bibi miguu na baba
na wazee wengine moyo na mgongo.
Ikibainika
mmoja amekula sehemu ya nyama ya kundi fulani inaweza kuleta ugomvi mkubwa na
hata aliyekula atakwenda kuinunua dukani na atashitakiwa kwenye vikao vya
familia.
Mgeni wa
heshima anapotembela rafiki yake anachinjwa mbuzi, ng’ombe au kuku lakini moja
ya sharti ni kwamba kama amechinjiwa yeye lazima ale filigisi na asipoiona
mezani atasusa kula.
Nguo- Asili ya nguo za kabila la
Wangoreme enzi hizo zilikuwa ni ngozi za wanyama hasa mbuzi na swala ambapo zilikuwa zinaambwa na kuondolewa
nywele zote na aliyeruhusiwa kuzivaa ni kijana mwenye umri miaka 18 na
kuendelea lakini baada ya nguo kuja walianza kuvaa hadi leo.
Silaha-Silaha kubwa ya kabila la Wangoreme ni upinde na mikuki
ambapo mafunzo ya kutumia zana hizo hufanyika wakati wa jando.
Ili
kuhakikisha umekuwa hodari na mtaalamu wa silaha hizo lazima vijana hao
wanaagizwa hifadhini kuwainda wanayama na kuleta nyama nyumbani.
Msiba,wizi- Wakati wa msiba, watu wote wa jirani
na ndugu hujumuika pamoja kushiriki mazishi.
Lakini mzee anapofariki asiyekuwa na mali mara
nyingi anazikwa kama alivyozaliwa na ili kuepusha kuzikwa hivyo huwa na
utaratibu wa kuweka mtoto wake wa kike rehani kwa mtu mwenye uwezo ili ampe
ng’ombe ya kushughulikia msiba.
Mtoto
anapokuwa mkubwa ataolewa na kijana wa yule aliyetoa msaada kwa familia ya
marehemu aidha kwa kuongeza mahali nyingine au ile ya awali inategemea na
wakati uliopo.
Kwa upande wizi
unapotokea ndani ya kabila la Wangoreme lazima itapigwa baragumu ikiashiria
hatari na watu wote huondoka nyumbani na upinde, mikuki wakiwa tayari kwa lolote.
Nyumba, Vitanda-Nyumba za asili za Kabila la
Wangoreme ni msonge ambazo zinajengwa na miti lakini kwa upende wa mwezekaji
nyasi hutafutwa mtaalamu ili kuzuia maji ya mvua yasiingie ndani.
Kwa upande
wa vitanda vya asili ni kuunganishs miti kwa mfani wa kitanda cha kisasa lakini
panapotakiwa kuweka change inaambwa ngozi ya ng’ombe.
Nyimbo
Pia nyimbo
zao za asili ni zeze na ngoma aina ya mbegete, kinanda, lukana ambapo
zinapopigwa huchezeshwa mabega huku wanawake
na wanaume husogeleana kwa kukusana vifua.
Maoni -O769 688300
================
MIPAKA YA VIJIJI ITATUGHARIMU BAADAYE
Mapigano ya
mipaka ya majimbo yazuka Mara
*RC aizuia tume
ya wizara
*Asema ilienda
kinyemela
*Wassira, Dk.
Kebwe wanena
*Mipaka
yang’olewa
*Wananchi
waahidi kumwaga damu
Na Benjamin Masese, Dar es Salaam
MAJIMBO matatu ya
wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara yameingia katika mvutano mkali wa kugombea mipaka yao huku dalili za wazi za wananchi kushika
mapanga, mishale na upinde zikianza kuonekana.
Mipaka hiyo ni ile
inayotenganisha Wilaya ya Musoma Vijijini, Serengeti, Bunda ambayo inahusisha vijiji vya Sirori
Simba(Musoma Vijijini), Remng’orori (Serengeti) na Mekomariro (Bunda).
Mgogoro wa mipaka hiyo ulianza kuibuika kwa mara ya
kwanza mwaka 1978 lakini hakuna
suluhisho lililopatikana licha ya mikutano kadhaa kufanyika ikiwahusisha viongozi
ngazi ya mkoa.
Waliovamia maeneo ya mipaka hiyo ni wafugaji, wakulima huku wakianza kuweka
makazi ya kudumu na shughuli za kijamii ambapo pande zote zikidai yuko Wilaya yake.
Dalili za
kuanza mapigano hayo zilianza kuonekana mwanzoni mwa mwezi huu baada ya
wananchi wa Wilaya ya Musoma Vijijini kung’oa mabango ambapo wananchi wa Wilaya ya Bunda wao
wakichimba mitaro na kuweka alama za mipaka inayowatenganisha na Wilaya ya Serengeti na Bunda huku wakitoleana
vitisho.
DC Serengeti
Akizungumza
na MTANZANIA juzi kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Joshua Mirumbe alikiri kuwapo na mgogoro huo huku
akisema kuwa umeanza kushughulikiwa na ngazi zote.
“Ni kweli
upo mgogoro huo naohusisha wilaya tatu lakini kutokana na uzito wa suala hilo tayari tume imetoka
Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuja kushughulikia
mipaka hiyo.
“Hivi
tunavyozungumza viongozi ngazi ya mkoa, wilaya, kata, tarafa, vijiji
wanashirikiana pamoja kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake bila kuingia katika
mapigano,”alisema kwa ufupi.
RC Mara
Akizungumza jana kwa njia simu, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel
Tupa alikiri kuwapo na mgogoro huo huku akiwaomba wananchi kutoingia kwenye
mapigano ya wao kwa wao kwa kuwa athari yake ni kubwa.
“Mgogoro huu ni mkubwa na ndio maana watalaam kutoka makao
makuu ya Wizara ya Ardhi wameletwa ikiwa lengo ni kupata suluhisho
lisilopendelea upande mmoja.
“Hasira za wananchi zilitokana na watalaam hao kwenda kwa
wananchi bila kuwa na wakuu wa wilaya zote tatu huku wakitumia jina langu
kwamba nimewaagiza.
“Kwa kweli walikosea na ndio maana nimewasimamisha kwanza na
kuwaagiza wakuu wa wilaya wazungumze nao kwa kuwapa elimu na kuwashauri watoe
ushirikiano ili wote kwa pamoja tupate suluhisho la kudumu.
“Kikubwa ninachosema ni kwamba uamuzi wa mgogoro huu upo mikononi
mwao lakini kama wamejiandaa na mapiganoya mikuki, mishale na mapanga ni
kuongeza tatizo.
“Nawasihi watoe ushirikiano kwa kuwa kamati zote zitaundwa na wao ambapo watatoa historia yote ya mipaka
kwa tume ya wizara ili kupata taswira halisi, pia nawaomba wananchi kuwa na
subira hadi tume itakapokamilisha kazi yake,”alisema.
Mwenyekiti Remng’orori
Kwa upande
wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Remg’orori, Justen Mgaya Baritile alisema mgogoro huo umedumu kwa miaka mingi.
Baritile
alisema kuwa mipaka iliyokuwa ikitambulika tangu enzi hizo ni ile ya mwaka 1978
lakini umekuwa ukisusua kupata suluhisho la kudumu.
Alisema
baada ya mgogoro huo kuibuka tena mwaka 1996 kulifanyika mkutano katika eneo hilo la mipaka
iliyohusisha viongozi wote ngazi ya mkoa, wilaya na wananchi wa pande zote tatu
hazikuafikiana.
Licha ya
kutoafikiana katika mkutano huo, maafisa watendaji wa kata inadaiwa walisaini
makubaliano hayo bila wananchi kuiridhia.
Baritile
alisema kuwa mgogoro huo tena uliibuika mwaka 2002 ambapo kulifanyika mkutano eneo hilo hilo na
kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Thomas Loi Sabaya (wakati huo), Mkuu
wa Wilaya ya Bunda, Hawa Mchopa ambaye pia alihudhuria kama Kaimu Mkuu wa mkoa
wa Mara.
Alisema
mkutano huo ulikaa Februari 28 ,2002
ambapo walipendekeza kuwa mpaka wa Bunda na Serengeti utapita kuanzia mto
mwikoma, Nyagubesi, Nyabetunguri, mlima bikaili hadi jiwe moja, Kewaiwai, Bonde
la mtemi Makongoro hadi Mto Tirina.
Mpaka kati
ya Serengeti na Musoma Vijiji walipendekeza kupita Kijiji cha Sirori Simba eneo
la Bonde la Nyagubesi, Nyabetunguri,
mlima Buruta hadi palipowekwa vibao vya Tanroad barabarani kama
ishara ya mwisho wa jimbo la Musoma
Vijijini.
Alisema kuwa
licha ya kukubaliana lakini mgogoro huo uliendelea kufukuta na kulazimika tena
kukaa mkutano Desemba 12, 2002 na kuhudhuria na viongozi wa ngazi kuanzia mkoa
hadi kijiji ambapo waliwatumia wazee maarufu na wa kale ili kutoa historia.
Hata hivyo
taarifa
Kwa Mwenyekiti (0786480194) wa Kijiji cha Sirori Simba,
Alexander Makile Nyangalesi alisema kuwa maamuzi yatakayotolewa na tume
yatakuwa ni sahihi.
Wassira
Kwa upande
wa Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Steven Wassira alikiri kuwapo na mgogoro huo
huku akienda mbali na kusema unahusisha wilaya nne yaani Serengeti, Bunda,
Butiama na Msoma Vijijini.
Wassira
ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Rais, alisema migogoro yote ya wilaya hizo inahusu
mipaka ambayo inapaswa kutenganisha Serengeti na Bunda, Serengeti na Musoma
Vijijini na Butiama na Bunda.
Wasira
alisema kuwa mipaka ya Wilaya ya Serengeti, Bunda na Butiama inahusisha vijiji
vya Mikomariro, mahanga na Ikizu ambapo upande Musoma Vijijini na Serengeti
unahusisha kijiji cha Sirori Simba na Remng’orori.
Pamoja na
ufafanuzi wake, alisema mipaka hiyo itapata muafaka kwa kurejea historia ya
tangu watawala wa ‘machifu’ walivyokuwa
wakitawala.
Wassira
alipinga vikali juu ya tuhuma dhidi yake kwamba anawatumia matajiri
wa jimbo lake
kuendeleza mapambano ya
kumega ardhi ya Serengeti.
“Sina nia ya
kuchukua ardhi ya Serengeti, hayo ni mawazo potofu ya wenye nia mbaya na
mimi,kwanza kwenye jimbo langu sina matajiri na wananchi wangu ni wa hali ya
kawaida.
“Kwanza
mipaka ya wilaya hizo iliwekwa wakati mimi nikiwa Mkuu wa Wilaya, sasa kama nilikuwa na nia hiyo ningetumia mwanya huo, suala la
watu kunichafua kwenye mitandao ya kijamii ni ijinga, tushirikiane kupata
muafaka,”alisema.
Dk. Kebwe
Kwa upande
wa Mbunge wa Serengeti, Dk. Kebwe Steven Kebwe alisema kwa ufupi
kwamba ana imani na tume itamaliza mgogoro huo.
Kuhusu tuhuma
za wananchi wakewakidai kushindwa kuitetea ardhi yao,
alisema kuwa hatua ya tume kwenda eneo hilo
ni jitihada zake na vikao vyote vya RCC kilichokaa Oktoba 17,2012 aliwatetea
wananchi juu ya mipaka hiyo.
MWISHO
Subscribe to:
Posts (Atom)