Sunday 25 August 2013

OPERESHENI YA KUONDOA POLISI WASIOFAA

Na Benjamin Masese, Dar es Salaam WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi ametembeza panga kali ndani ya Jeshi la Polisi na kuwafukuza kazi maofisa wanne huku baadhi yao wakivuliwa vyeo vyao. Maofisa hao ni wale waliohusika kushiriki kwa namna moja au nyingine katika matukio yaliyotokea mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma na kulalamikiwa vikali na wananchi. Akizungumza na Waandishi wa habari Da r es Salaam jana alisema askari hao ni wale waliohusika kutumia gari la kutuliza Ghasia (FFU) kubeba bangi mkoani Arusha na Kilimanjaro Tukio jingine ni lile la askari mkoani Morogoro kutumia fuvu la binadamu kumbambikizia mfanyabishara kwa lengo la kupata fedha, mauaji ya mfanyabishara wa Wilaya ya Kasulu yalifanywa na askari polisi. Tukio la Bangi Dk. Nchimbi alisema katika sakata la tukio la bangi amemvua madaraka yote aliyokuwa nayo Mkuu wa Kikosi cha FFU Mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi, Ramadhan Giro kwa kosa la kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maofisa walio chini yake na kusababisha kutoke tukio hilo. Pia amemsimamisha kazi Ispekta Isaac Manoni na kushitakiwa kijeshi kwa kosa la kutumiwa kumtorosha mtuhumiwa ambaye ni polisi Edward Mwakabonga aliyekuwa dereva wa gari la FFU kitendo kilicholifedhehesha jeshi hilo. “Katika tukio hilo kitendo cha Inspekta Salum Kingu wa kikosi cha FFU Mkoa wa Kilimanjaro kubaki kwenye gari mita 80 kutoka ilipo nyumba ya mtuhumiwa Edward alipopelekwa Moshi kukabishi vifaa vya jeshi letu kimechangia, hivyo tumempa onyo kali la kuwa makini na utendaji wake. “Pia Inspekta Mikidadi Galilima kutotimiza wajibu wake ipasavyo katika kumshauri Mkuu wa FFU Mkoa wa Arusha juu ya ukaguzi na usimamizi wa rasilimali na kujaribu kuficha ukweli wa tukio, nimempa onyo kali Inspekta Galilima. “Katika tukio hilo nimempandisha cheo ASP Francis Duma aliyekuwa kiongozi wa askari 14 katika kupambana kulikamata gari la FFU lililobeba bangi na kuwa Mrakibu wa Polisi,askari wengine 14 nimegiza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Said Mwema kuwapandisha vyeo kwa sababu wapo ngazi yake,”alisema. Tukio la fuvu Dk. Nchimbi alisema amewavua madaraka yote waliyonayo Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Mvomero, Inspekta Jamal Ramadhan na Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila, Inspekta Juma Mpamba kutokana na kuonyesha udhaifu mkubwa katika utendaji kazi wa kushindwa kuwasimamia askari wake na kushindwa kuwakamata matapeli na hawalifu ambao ni vinara. Dk. Nchimbi alisema kabla ya tukio la askari watatu kushirikiana na raia wawili kumbambikizia fuvu la binadamu mfanyabishara Samson Mwita, Inspekta Ramadhan alikuwa na taarifa za mpango wa tukio hilo la askari wake kushirikiana na rai kufanya kufanya hivyo lakini hakumtaarifa Inspekta Mpamba. Alisema askari wote waliohusika na tukio hilo ambao ni Sajeti Pasua Mohamed, Sajeti Sadick Madodo Koplo Nuran Msabaha wamefukuzwa kazi na kushitakiwa kwa uhalifu waliotenda sambamba na raia wawili ambao ni Rashid Hamisi na Adamu Peter. Kupiga na kuua raia Dk. Nchimbi alisema Disemba 25 mwaka jana askari wa kituo kidogo cha polisi cha Heru Ushingo kilichopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa pamoja walimpiga raia ambaye ni marehemu sasa Gasper Sigwavumba na kumweka mahabusu bila msaada wowote wa matibabu. Alisema katika tukio marehemu alipasuka bandama kutokana na kipigo hicho na kuongeza kwamba upelelezi mbovu uliofanywa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu, ASP Daniel Bendarugaho kesi ya mauaji iliweza kuondolewa mahakamani. Dk. Nchimbi alisema wakati kesi inaondolewa mahakamani askari waliohusika ambao ni Koplo Abraham Peter na PC Simon Sunday walikuwa wamefukuzwa kazi na kuwa huru jambo ambalo lilizua malalamiko. “Kutokana na ASP Bendarugaho kutokuwa makini katika kusimamia upelelezi wa jalada husika la kesi hiyo ya mauaji tunavua madaraka na upelelezi unaanza upya ili haki itendeke,”alisema. “Operesheni ya kulisafisha jeshi hilo itaendelea hadi litakapokuwa safi, leo hii wananchi wamekata tama kabisa na jeshi la polisi ukimwambia kitu chochote juu ya polisi haamini. “Kwa kipindi nitakachokuwa naongoza wizara hii, nitalisafisha na Watanzania watarudisha imani kwa polisi, katika matukio haya matatu askari waliohusika moja kwa moja wamefukuzwa kazi na kushitakiwa. “Haya ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa na timu niliyoiunda ambapo Mwenyekiti wake alikuwa Mkurugnezi Mkuu wa Idara ya masuala ya Malalamiko Makao Makuu, Augostine Shio.

1 comment:

  1. Wynn casino in Las Vegas, Nevada - JRM Hub
    Wynn Resort Hotel, Casino & Spa features luxurious 창원 출장마사지 bedding, an oversized 속초 출장마사지 flat-screen TV, 제주 출장샵 and a seating 논산 출장안마 area. Located in the 서귀포 출장마사지 center of the Las Vegas Strip,

    ReplyDelete